Uhasi Wazi Wa Maudhui Katika Tamthilia Teule Za Kiswahili Nchini Kenya.
Abstract
Tamthilia ni mojawapo ya tanzu za fasihi andishi zinazofundishwa katika shule za upili nchini Kenya. Tamthilia pia hutahiniwa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne nchini Kenya Utanzu huu huandikwa kwa mtindo wa mazungumzo kama mchezo wa kuigizwa. Mojawapo kati ya malengo ya elimu nchini Kenya ni ufungamano wa kitaifa. Kila kipengee cha elimu nchini, hupaswa kuelekezwa katika kutimiza malengo ya elimu kama yanavyodokezwa na KIE (2006). Makala haya yanatathmini jinsi suala la ufungamano wa kitaifa limeshughulikiwa na tamthilia zinazotahiniwa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne. Lengo kuu la makala haya ni kuchunguza iwapo tamthilia teule zimesawiri kichanya maudhui yanayohusu suala la ufungamano wa kitaifa na nafasi inayochukuliwa na migogoro na maridhiano katika tamthilia teule kwa shule za upili nchini Kenya.
Istilahi muhimu: tamthilia, usawiri, uchanya, uhasi, migogoro, maridhiano, ufungamano, taifa na jamii.
To list your conference here. Please contact the administrator of this platform.
Paper submission email: JEP@iiste.org
ISSN (Paper)2222-1735 ISSN (Online)2222-288X
Please add our address "contact@iiste.org" into your email contact list.
This journal follows ISO 9001 management standard and licensed under a Creative Commons Attribution 3.0 License.
Copyright © www.iiste.org